Kutuma Pesa Kutoka TIGO-PESA kwenda Benki ya CRDB kwa kutumia Huduma za Kifedha
- Kwenye sehemu ya kupigia simu andika *150*01# na ubofye kidude cha kupigia simu
- Chagua namba 6 Huduma za Kifedha
- Chagua namba 1 TIGO-PESA kwenda Benki
- Chagua kwenye orodha ya mabenki namba moja (1) kwa maana ya CRDB
- Chagua moja (1) Kuingiza namba ya kumbukumbu
- Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (Tumia akaunti namba ya benki)
- Weka kiasi
- Ingiza namba ya siri kuhakiki
Subiri ujumbe kutoka TIGO na CRDB wa kukujulisha kama muamala wako umefanikiwa na kama haujafanikiwa rudia tena kwa kuanza na hatua ya kwanza hapo juu