GLORIA MUNHAMBO: : NINATAKA KUINGIA MJINI KWA MUNGU

Solo: Ninataka kuingia mjini kwa Mungu,ninakaza nitashinda mwendo nifike

Wote: Nikishikwa na shida,nikichoka njiani,Yesu unaniambia ?Uningojee? x2

Solo: Naitwa na Yesu Kristo ,enzini mwake,nakimbia, kukawia,hakuna faida

Wote: Wote wachelewao,hawatapata taji,mimi sitaki kingine, ila uzima x2

Solo; Elekeza macho yangu,langoni mwako,niongoze,nipe nguvu,ninapochoka

Wote: Ninapojaribiwa,ninapozingiziwa,Yesu unisaidie,nisikuache x2

Solo: Mkono wako unishike nisianguke,Najiona kuwa mnyonge,nguvu I kwako

Wote: Neno lako ee Yesu linanipa uzima,nikifika nitaimba umeniponya x5